top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 16 Oktoba 2024

Vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea ndani ya kuta za tumbo na huhushisha umio yaani mrija unaoingiza chakula kwenye tumbo, tumbo ama na Duodenamu ambapo ni sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba mara baada ya tumbo.

 

Hivo vidonda vya tumbo huweza kugawanya katika aina tatu

 

1.vidonda ndani ya mrija unaopeleka chakula kwenye tumbo (esophagus)

2.vidonda vya tumbo ndani ya tumbo(gastric)                                                  

3. Na vidonda vya tumbo kwenye mrij unaotoa chakula katika tumbo ama (duodenum)

 

Kwa sasa madaktari wanajua kwamba  maambukizi ya bakiteria au baadhi ya madawa yanaweza kusababisha vidonda vya tumbokwa asilimia kubwa zaidi ukilinganisha na chakula na ama msongo wa mawazo

 

Dalili za vidonda vya tumbo

​

Maumivu ya tumbo huwa ni dalili kuu, maumivu haya huwa ya aina ya kuunguza. Maumivu hayo hutokana na vidonda haswa pale tindikali iliyopo tumboni inapokutana na vidonda hivo na kuviunguza zaidi

​

Maumivu hayo yanaweza;

  • Kutokea sehemu yoyote kati ya  kitovu na sehemu ya kifua karibu na chuchu

  • Kuongezeka ukila chakula

  • Kupungua ukila chakula

  • Kuongezeka wakati wa usiku

  • Kupungua kwa muda unapokula vyakula ama vinavyopunguza makali ya tindikali tumboni ama unapotumia dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni

  • Kupotea na kutokea baada ya siku/wiki chache baadae

                                                  

Dalili zingine za vidonda vya tumbo ni kama vile

​

Kwa mara chache sana  vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha dalili kali sana kama vile

  • Kutapika damu-nyekundu ama nyeusi

  • Kinyesi kuwa cheusi kinaweza kuwa cheusi kama rami pia

  • Kichefuchefu na Kutapika

  • Kupoteza uzito bila sababu

  • Kubadilika kwa hamu ya kula


Vidonda vya tumbo

​

Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea ndani ya kuta za utumbo kuanzia kwenye mpira unaoingiza chakula kwenye tumbo, tumbo ama na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba mara baada ya tumbo. Hivo vidonda vya tumbo huweza kugawanya katika aina tatu

​

1.vidonda ndani ya mrija unaopeleka chakula kwenye tumbo (esophagus)

2.vidonda vya tumbo ndani ya tumbo(gastric)                                                  

3. Na vidonda vya tumbo kwenye mrij unaotoa chakula katika tumbo ama (duodenum)

 

Nini husababisha vidonda vya tumbo?

 

Vidonda vya tumbo hutokea endapo tindikali ndani ya utumbo  zitapenyeza na kula ukuta wa ndani wa tumbo na kuleta vidonda katika maeneo kabla ya tumbo tumboni na baada ya tumbo. Mfumo wa tumbo umefunikwa kwa juu na ukuta wa uteute kama mlenda ambao huzuia tindikali hizi kupenyeza na kula nyama za kuta za tumbo. Hivo kama uteute huu ukipungua ama kama uzalishaji wa tindikali ukiongezeka basi mtu anaweza kupata vidonda vya tumbo. Sababu kuu  zinazoweza kusababisha ni;

  • Maambukizi ya bakiteia aina ya H pylori. Bakteria huyu huishi katika uteute ambao hufunika kuta za juu za tumbo dhidi ya muunguzo wa tindikali. Bakiteri ahuyu huwa na tabia ya kuzalisha baadhi ya vimiminika ambavyo huharibu uteute huu na kusbabisha kuunguzwa kwa ukuta wa juu wa tumbo na kuleta vidonda vya tumbo. Pia bacteria huyu huweza kuzunguka katika uteute na kusababisha mashimo ambayo tindikali hupita na kuunguza ukuta wa tumbo

  • Chakula na dawa- Baadhi ya vyakula na dawa huweza kusababisha vidonda vya tumbo endapo zitatumiwa kwa mda mrefu, dawa hizi ni zile za kuondoa maumivu na ni jamii aina ya (NSAID)aspirini, kama aspirini, diclofenac,ibuproren, naproxen ketoprofen na zingine jamii hii

    • Vidonda vya tumbo hutokea sana kwa wazee wanaokunywa dawa hizo kwa sababu ya kuondoa maumivu ya viumgo vya mwili ama wanaotumia kwa ajili ya tatizo la osteoarthritis.

    • Dawa zingine zinazotibu osteoarthritis yanayoweza kusababisha vidonda vya tumbo ni kama vile biphosphonate na virutubisho vya potassium

​

  • Kurithi uzalishaji tindikali wa kiwango cha juu. Kuna baadhi ya watu wanatatizo la uzalishaji wa tindikali kwa wiki katika kuta za tumbo , hali hii inasababisha kuungua kwa kuta za tumbo na kupelekea tatizo la vidonda vya tumbo

  • Kuwa na Saratani katika chembe zinazozalisha tindikali tumboni.

​

Vihatarishi vya kupata vidonda vya tumbo

 

  • Uvutaji wa sigara

  • Unywaji wa pombe--huchoma na kusababisha vidonda katika tumbo na pia huongeza uzalishaji wa tindikali

  • Madhara ya vidonda vya tumbo

  • Huweza kupelekea

  • Kutoboka kwa kuta za tumbo-kusababisha maumivu makali sana ya tumbo ambayo hujawahi yasikia

  • Kuvuja kwa damu ndani ya tumbo

  • Maambukizi ndani ya ukuta unaofunika matumbo

  • Makovu ndani ya tumbo

​

Vipimo na matibabu

 Yapo matibabu ya aina tofauti, hutegemea ni nini kinachosababisha tatizo hili kutokana na vipimo vilivyofanyiaka

Vipimo vinavyoweza kufanyika ni kama vile

Kipimo cha kutambua uwepo wa bakiteria wa H pylori kwenye damu, kinyesi ama kipimo cha kutambua gesi aina ya urea kwenye pumzi ambayo hutole na bakiteria huyu.


Kipimo cha kutumia kamera inayoonyesha mfumo wa tumbo ama endoscope- ni kizuri kwani huonesha kidonda kilipo na kuchukua kinyama kwa ajiri ya uchunguziKipimo cha Xray endapo unadalili za kutoboka kwa ukuta wa tumbo 

Dawa zinazotumika

​

  • Dawa za kutibu maambukizi ya bakiteria wa Hpylori

  • Dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali

  • Dawa za kusiamisha uzalishaji wa tindikali

  • Dawa zinazopunguza makali ya tindikali iliyozalishwa

  • Dawa zinazoongeza uteute katika kuta za tumbo

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

16 Oktoba 2024, 05:51:20

Rejea za mada hii:

​Peptic ulcer disease and H. pylori. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/digestive-diseases/peptic-ulcer/Pages/overview.aspx. Imechukuliwa 05.07.2020

Peptic ulcer disease and NSAIDs. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/digestive-diseases/peptic-ulcer/Pages/overview.aspx. Imechukuliwa 05.07.2020

Vakil NB. Epidemiology and aetiology of peptic ulcer disease. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 05.07.2020

Feldman M, et al. Peptic ulcer disease. In: Sleisenger and Fordtran's Gastrointestinal and Liver Disease: Pathophysiology, Diagnosis, Management. 10th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 05.07.2020

Rakel D. Peptic ulcer disease. In: Integrative Medicine. 3rd ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2012. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 05.07.2020

Feldman M, et al. Helicobacter pylori infection. In: Sleisenger and Fordtran's Gastrointestinal and Liver Disease: Pathophysiology, Diagnosis, Management. 10th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 05.07.2020

Ferri FF. Peptic ulcer disease. In: Ferri's Clinical Advisor 2016. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 05.07.2020

bottom of page