top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 25 Novemba 2020

Kipimo cha urine culture

Kipimo cha kuotesha mkojo ni cha umuhimu sana kwa mgonjwa mwenye U.T.I sugu au isiyosikia dawa. Kipimo hiki kina uwezo wa kutambua aina ya kimelea aliyesababisha maambukizi pamoja na dawa inayofaa kumwangamiza kimelea huyo.


Kuna hali mbalimbali zinazoweza kupelekea uhitaji wa kufanya kipimo cha urine culture ili kutambua maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo (U.T.I). Makala hii imezungumzia maana ya kipimo, kwanini na kwa jinsi gani kinafanyika na majibu yanapatikana baada ya muda gani.


Kipimo hiki ni nini?



Hiki ni kipimo cha mkojo kinachotumika kupima sampuli ya mkojo kwa kuotesha viini vya maradhi kutoka kwenye sampuli na hufanyika katika maabara maalumu zenye kiwango na zinazoruhusiwa kufanya kipimo hiki.


Umuhimu wa kipimo


Kipimo cha culture na sensitivity ni muhimu kufanyika ili;


  • Kutambua ni aina gani ya bakteria wanaosababisha maambukizi

  • Kufahamu ni aina gani ya dawa inaweza kuua bakteria waliosababisha UTI

  • Kutofautisha kuchafuliwa kwa sampuli kutoka kwenye bakteria wa ngozi ya maeneo ya siri


Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?


Watu wanaopaswa kufanya kipimo hiki ni wale ambao wana UTI sugu na ile ya kujirudia rudia


Aina ya sampuli inayotakiwa


Sampuli inayotakiwa kukusanywa ni mkojo


Malengo ya mkojo wa kipimo cha urine culture hutakiwa kukusanywa katika hali ya kuzuia mkojo huo kuchanganyika na bakteria wengine kwenye Ngozi ya maeneo ya siri. Jinsi ya kukusanywa imeandikwa hapa chini. Ni muhisu sana kwa mgonjwa kujifunza namna ya kukusanya mkojo ili majibu yake yaje sahihi.


Namna ya kukusanya sampuli


Ukusanyaji wa mkojo ni lazima uzingatie usafi wa sampuli na kwa kutumia kihifadhi sampuli ambacho kimetakaswa


Kwa wanawake

Mwanamke akiwa anakusanya mkojo anatakiwa kutanua mashavu ya uke kwa kutumia vidole viwili vya mkono mmoja ili mkojo usiguze Ngozi ya mashavu hayo.


Kwa wanaume

Endapo mwanaume hajatahiliwa atatakiwa kuvuta govi la uume nyuma kwanza ili kufanya mkojo utoke bila kukusa govi hilo.


Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine

Ukusanyaji wa sampuli ya mkojo kwa njia ya sindano

Kwa watu wenye maambukizi ya UTI kwenye kibofu, mkojo unaweza kukusanywa kwa kupitia sindano inayochomwa kwenye tumbo kuelekea kwenye kibofu haswa kwa watu ambao kipimo cha culture kilichofanyika kwa njia ya mkojo hakijaleta majibu ya kueleweka au ya kuchang’anya.

Watoto wadogo pia kwa sababu hawawezi kufuata maelekezo hayo ya juu, mkojo huweza kukusanywa kwa njia hii ya sindano.


Ngozi ya juu ya kibofu cha mkojo karibu na mfupa wa pubis itasafishwa vema na sindano itaandaliwa kwa ajili ya kuchoma kwenye maeneo ya suprapubic ili kuvuta mkojo kwenye kibofu. Kipimo cha Ultrasound kinaweza kuagizwa kufanyika ili kuhakikisha kwamba kibofu kina mkojo wa kutosha kabla ya kuchukuliwa kwa sampuli za mkojo


Ukusanyaji wa sampuli ya mkojo kwa kutumia catheter

Utaingiziwa catheter kwenye mrija wa mkojo, kisha mkojo kiasi utaachwa utoke, baada yah apo utakusanywa mkojo wa katikati katika kikopo cha kukusanyia sampuli kilichoandaliwa.


Njia hii ya ukusanyaji husemekana kuongeza bakteria wapya kwenye kibofu kutoka kwenye Ngozi ya maeneo ya nje kwa asilimia 1 mpaka 2 hata hivyo kiasi hiki ni kidogo kuzuia kuchukuliwa kwa sampuli ya kwa njia hii kwa wagonjwa ambao ni lazima sampuli ichukuliwe hivi.


Ukusanyaji wa mkojo wa wagonjwa wenye ilea conduit

Mkojo unaotoka kwenye kimfuko cha ilea conduit maranyingi huwa si msafi, mkusanyaji anatakiwa kuingiza catheter ndani Zaidi kwenye mirija ya mkojo ili kukusanya mkojo msafi.


Utunzaji wa sampuli


Kikopo gani cha sampuli kinatakiwa kutumika?


Kikopo cha kukusanyia mkojo kinatakiwa kuwa kilichotakaswa ili kuzuia mkojo wako kuchanganyika na bakteria wengine.


Muda wa sampuli kuwa hai


Sampuli inatakiwa kupimwa ndani ya masaa 12, baada ya hapo majibu hayatakuwa sahihi


Muda wa kupata majibu ya kipimo chako


Majibu hutegemea lakini huchukua kuanzia masaa 24 hadi 72


Usomaji wa majbu


Majibu yatasomwa na daktari aliyeagiza kufanyika kwa kipimo hiki


Endapo bakteria wamekuwa kwa kiasi Zaidi ya 105CFU/mL itatosha kusema kuwa una maambukizi ya UTI, hata hivyo endapo kipimo kinasoma kwamba viini vya maradhi vimeota kati ya 102-104CFU/mL jumlisha dalili za UTI kwa wanawake, itasemekana pia kuwa una UTI na utatakiwa kutibiwa.


Kuota kwa vimelea wachache chini ya 104CFU/mL kwa wanaume inatosha pia kusema kwamba una UTI kwa sababu kwa wanaume ni ngumu sana mkojo kuchanganyika na viini kutoka kwenye ngozi yua maeneo ya siri.


Viini vya aina tofauti vinaweza kuota kwenye kipimo hiki bila kuwa na wasiwasi wa kuchanganywa kwa viini vya maradhi wakati wa kukusanya mkojo endapo njia ya mkojo imeziba au kuwa na kitu kigeni ndani ya njia na kibofu cha mkojo


Majibu chanya

Majibu chanya huonyesha kuota kwa bakteria anayesababisha maambukizi pamoja na kuonyesha dawa gani yenye uwezo mkubwa wa kuua bakteria na zipi ambazo hazina uwezo wa kumuua bakteria. Baadhi ya maelezo ya majibu yameandikwa hapo juu.


Majibu hasi

Majibu hasi hutokea pale endapo mkojo haukuwa safi au kuchanganyika na bakteria wa kwenye ngozi. Wakati huu kipimo hiki cha culture kinatakiw akurudiwa fanyika tena na umakini katika ukusanyaji wa sampuli unatakiwa kuzingatiwa. Baadhi ya maelezo ya majibu yameandikwa hapo juu.


Ushauri wa msingi kwa mgonjwa


Mgonjwa unashauriwa kuzingatia umakini katika ukusanyaji wa sampuli.

ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.

ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.

Imeboreshwa,

8 Novemba 2021, 10:49:35

Rejea za mada hii

  1. Oxford Handbook of Clinical and Laboratory Investigation, 4th edition. 2018. By Drew Provan. ISBN 978–0–19–876653–7. 

  2. Full blood count. http://www.bbc.co.uk/health/talking/tests/blood_full_blood_count.shtml. Imechukuliwa 24.11.2020

  3. Full blood count. http://www.rcpa.edu.au/pathman/full_blo.htm. Imechukuliwa 24.11.2020

bottom of page