top of page

Vipimo vya maabara

Katika kurasa hii utafahamu kuhusu vipimo mbalimbali, namna vinavyofanyika, kwanini vinafanyika na majibu pia yanasomwa vipi. Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa tu.

Kipimo cha wingi wa damu (hemoglobin)

Kipimo cha wingi wa damu (hemoglobin)

Kipimo cha wingi wa damu kwa jina jingine 'kipimo cha hemoglobin', hupima idadi ya protini ya hemoglobin iliyo ndani ya chembe nyekundu za damu. Mgonjwa anayepaswa kufanya kipimo hiki ni yule mwenye dalili za uchovu mkali, kuishiwa pumzi na kizunguzungu, aliyeongezewa damu na anayetarajia kufanyiwa upasuaji.

Kipimo cha antijeni za H. pylori

Kipimo cha antijeni za H. pylori

Kipimo cha kutambua antijeni za H. pylori hutumika kuchunguza uwepo wa protini za bakteria Helicobacter pylori kwenye kinyesi. Uchunguzi huu humwezesha daktari kufahamu kama vidonda vya tumbo vimesababishwa na bakteria huyu au la.

Kipimo cha peripheral blood film

Kipimo cha peripheral blood film

Kipimo hiki hutumia hadubini kutazama chembe nyekundu za damu zilizotiwa rangi (stain) ili kuona vema chembe nyekundu, nyeupe na chembe sahani za damu.

Kipimo cha Full blood picture- FBP

Kipimo cha Full blood picture- FBP

Kipimo chA CBC huwa ni kipimo muhimu sana kwa dunia ya sasa kwani husaidia wataalamu wa afya kupata fununu za nini kinaendelea ndani ya mwili pamoja na kutambua magonjwa mbalimbali.

bottom of page