Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Charles W, MD
27 Septemba 2021, 07:24:18
Kirusi Rubella
Kirusi Rubella ni aina ya kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Rubella. Kirusi hiki husababisha homa na vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi hiki husababisha homa na vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani.
Ugonjwa wa Rubella umeanza mwaka gani?
Ugonjwa wa Rubella ulianza mwaka 1962. Waliogundua ugonjwa huu walikuwa makundi mawili tofauti ambao ni Paul D. Parkman na wenzake pia Thomas H. Weller na Franklin A. Neva.
Kirusi Rubella kipo katika Familia gani?
Kirusi Rubella ni kimoja wapo kwenye genus ya Rubivirus na familia ya Togaviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi.
Sifa za kirusi
Kirusi Rubella ni kirusi cha strendi moja ya RNA hasi.Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Togaviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana strendi moja ya RNA hasi
Wana umbile lenye pande 20 (icosahedral)
Ukuta wa njee wa seli ya bakteria imejifunga
Wana kipenyo cha 70nm
Makundi ya familia ya Familia
Familia ya Togaviridae imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni;
Alphavirus
Rubivirus
Virusi wengine walio kundi moja na Kirusi Rubella ni;
Eastern Equine encephalitis virus
Western equine encephalitis virus
Venezudan equine encephalitis virus
Chikungunya virus
River virus
Barmal forest virus
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Rubella hutunzwa na binadamu, nguruwe na farasi.
Kirusi Rubella kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Rubella kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua.
Wakati mwingine watu huambukizwa Rubella wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni.
Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Dalili za ugonjwa wa Rubella
Muda wa kuatema (incubation period) ni ndani ya siku kumi na nne mpaka siku ishirini na moja. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine hata kabla dalili hazijaonekana;
Dalili za ugonjwa wa Rubella ni;
Joto la mwili kupanda
Mwili kuchoka
Kuhisi baridi
Kichwa kuuma
Maumivu ya koo
Mafua
Vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani
Kukosa hamu ya kula
Macho kuwa mekundu
Tezi kuvimba
Kichefuchefu
Vipimo
Vipimo vya Ugonjwa wa Rubella;
Picha nzima ya damu
Kuotesha virusi
Serological tests
Immunofluorescent assay
Latex agglutination test
Elisa test
Hemagglutination inhibition test
Magonjwa yanayofanana na maambukizi ya kirusi rubella
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Rubella ni;
Herpes Virus 6 infection
Measles
Parvovirus B19 Infection
Pediatric contact dermatitis
Pediatric cytomegalovirus infection
Pediatric enteroviral infection
Pediatric mycoplasma infection
Pediatric syphilis
Toxoplasmosis
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa wa Rubella ni;
Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa wa Rubella ila mgonjwa anaweza kufanyiwa yafuatayo;
Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa.
Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu
Mgonjwa anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mgonjwa anatakiwa anywe maji mengi ya kutosha
Mgonjwa anatakiwa apate chanjo kama bado hajapata chanjo
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kujikinga na kirusi Rubella;
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu.
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye.
Pata chanjo ya Rubella kwa wakati sahihi.
Nawa mikono yako mara kwa mara.
Chanjo
Je kuna chanjo ya kirusi Rubella?
Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rubella ipo na hutolewa mtoto akiwa na miezi 12 hadi miezi 15 pia atapata chanjo nyingine kwenye umri wa miaka 4 hadi miaka 6.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
​
Rejea za mada hii;
MAYO CLINIC. Rubella virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/rubella/diagnosis-treatment/drc-20377315. Imechukuliwa 23/09/2021.
SCIENCE DIRECT. Rubella Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/togaviridae. Imechukuliwa 23/09/2021.
MEDSCAPE. Â Rubella Virus. https://emedicine.medscape.com/article/968523-overview. Imechukuliwa 23/09/2021.
CDC. Rubella virus. https://www.cdc.gov/vaccines/pubs/pinkbook/rubella.html#rubella-virus. Imechukuliwa 23/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:05:27