Mwandishi;
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri;
Dkt. Helen A, MD
4 Juni 2023, 13:27:14

Aina za VVU
Je, kuna aina tofauti za VVU?
Je, VVU huathirije mwili?
Kuna aina mbili za VVU, VVU-1 na VVU-2, pamoja na anuai kadhaa zinazohusiana ambazo huambukiza nyani aina fulani na sokwe mtu. VVU-1 vinaweza kupatikana duniani kote, lakini VVU-2 hupatikana tu Afrika Magharibi. VVU-1 huambukizwa kwa urahisi zaidi kuliko VVU-2, na maambukizi ya VVU-1 huwa na kasi zaidi ya kusababisha UKIMWI.
VVU huambukiza chembe za mfumo wa kinga ya binadamu, hasa aina ya chembe nyeupe ya damu inayoitwa chembe CD4 T. Chembe hizi husaidia katika kutambua na kuharibu vitu vyenye madhara mwilini, vikiwemo bakteria, virusi, vimelea na hata baadhi ya chembe za saratani. Baada ya muda, maambukizo ya VVU huharibu chembe za CD4, na kusababisha mfumo dhaifu wa kinga. Aina fulani za maambukizi huweza kushambulia mwili na kusababisha kifo, huwapata walioathirika kwa kipindi hiki. Maambukizi hayo mara nyingi huitwa "maambukizi nyemelezi" kwa sababu ni nadra au ni hafifu kwa watu wenye afya nzuri lakini yanaweza kutumia fursa iliyotolewa na mfumo wa kinga uliodhoofiwa na VVU na inaweza kutishia maisha. Virusi vya UKIMWI pia vinaweza kuharibu tishu moja kwa moja, na kusababisha ugonjwa wa neva, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine.
Hesabu ya chembe za CD4 (wakati mwingine huitwa hesabu ya chembe T) ni kipimo cha idadi ya chembe za CD4 katika mikrolita moja ya damu. Watu wenye VVU na wahudumu wao wa afya hutumia kipimo cha CD4 kufuatilia maambukizi kwa muda.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Kwa maelezo zaidi kuhusu virusi vya ukimwi soma makala ya Kirusi cha UKIMWI kwenye tovuti hii au kwa kusoma makala ya Maambukizi ya virusi vya UKIMWI au makala ya Dalili za Virusi vya UKIMWI.
Pia unaweza kutazama video mbalimbali kuhusu UKIMWI na Virusi vya UKIMWI
Dalili za awali za UKIMWI
Je Mtu anayetumia ARV huambukiza?
Vipele vya UKIMWI kwenye ngozi vikoje?
UKIMWI huonekana Baada ya Muda gani?
Kuwashwa mwili ni dalili ya UKIMWI?
PrEP Kuzuia Maambukizi ya UKIMWI
Imeboreshwa;
23 Julai 2023, 14:00:51