Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L, MD
5 Oktoba 2021 17:04:37
Human respiratory syncytial virus
Kirusi Human respiratory syncytial ni kirusi kinachosababisha maambukizi kwenye mfumo wa chini wa upumuaji hasa kwa watoto wadogo kabla hawajafikisha miaka miwili.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi hiki husababisha maambukizi kwenye mfumo wa chini wa upumuaji
Kirusi kilianza mwaka gani?
Kirusi human respiratory syncytial kigundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1956 wakati mtafiti alitoona kirusi katika majimaji kutoka kwa sokwe mtu aliyekuwa na dalili za ugonjwa wa mapafu na hivyo kuitwa jina la Chimpanzee Coryza Agent. Mwaka 1957 kirusi alitambuliwa kwa mtoto mdogo na kikaonekana kusababisha maambukizi wka watoto wadogo kabla ya kufikisha miaka miwili na hivyo kikapewa jina la human orthopneumovirus au human respiratory syncytial virus
Kirusi Human respiratory syncytial kipo katika Familia gani?
Kirusi Human respiratory syncytial ni kimoja wapo kwenye genus ya Orthopneumovirus na familia ya Pneumoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha maambukizi katika mfumo wa upumuaji.
Sifa za kirusi
Human respiratory syncytial ni kirusi chenye strendi moja ya RNA hasi katika familia ya virusi vya Pneumoviridae yenye sifa zifuatazo;
Strendi moja ya RNA
Urefu wa 15-28kb
Wana RNA hasi
Ukuta wa seli yake umefugwa
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Human respiratory syncytial hutunzwa na binadamu.
Kirusi Human respiratory syncytial kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Human respiratory syncytial kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua.
Wakati mwingine watu huambukizwa wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni.
Vihatarishi vya kupata maambukizi
Watoto wadogo wenye matatizo ya mapafu ya muda mrefu.
Mkusanyiko mkubwa wa watu
Mtu yeyote anayekaa karibu na mtu mwenye maambukizi.
Watu ambao kinga ya mwili imeshuka.
Watoto waliozaliwa kabla ya muda.
Watoto ambao hawajanyonya vizuri.
Watoto waliozaliwa zaidi ya wawili.
Uchafuzi wa mazingira.
Dalili za maambukizi ya kirusi Human Respiratory syncytial
Muda wa kuatema ni ndani ya siku tatu hadi tano. Mtu mwenye maambukizi ya kirusi respiratory syncytial huweza kumuambukiza mwingine hata kabla dalili hazijaonekana. Dalili za maambukizi ya kirusi respiratory syncytial;
Kikohozi
Homa
Kushindwa kupumua vizuri
Sayanosis
Mafua
Kuingia ndani kwa misuli ya kifua
Miruzi ya kifua
Sepsis
Rales
Vipimo
Picha nzima ya damu
Kuotesha kirusi
Polymerase chain reaction
Kipimo cha mkojo
Serum electrolyte concentration
Picha nzima ya kifua
Kipimo cha oxygen
Magonjwa yanayofanana
NImonia ya watoto
Bronkaitiz ya watoto
Sepsis kwa viachaga
Influenza
Bronnkolaitiz
Adenovirus
Croup
Human metapneumonia virus
Human parainfluenza virus
Matibabu
Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu
Mgonjwa dawa aina ya bronchodilator
Mgonjwa atapatiwa maji mengi kwa njia ya mshipa au kunywa
Mgonjwa atapatiwa Ribavirin kama antiviral
Mgonjwa atapatiwa oxygen endapo oxygen yake itakuwa chini
Je kuna chanjo ya kirusi Human Respiratory syncytial?
Mpaka sasa hakuna chanjo ya kirusi respiratory syncytial.
Kinga
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka
Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji safi na sabuni
Usiguse macho yako, pua na mdomo
Usikae karibu na mtu mwenye maambukizi
Imeboreshwa;
5 Oktoba 2021 17:31:41