Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. benjamin L, MD
27 Septemba 2021 07:01:33
Kirusi Hepatitis A
Kirusi Hepatitis A ni aina kirusi anayesababisha homa ya ini inayoweza kuwa ya wastani au kali na inayoweza kudumu kwa muda wa wiki chache au miezi kadhaa.
Ugonjwa wa homa ya ini A
Ugonjwa wa homa ya ini aina ya kirusi hepatitis A umeanza mwaka 1973 uko Purcell ambapo binadamu pekee ndio walionekana kuwa hifadhi ya virusi hawa.
Kirusi Hepatitis A kipo katika Familia gani?
Kirusi cha Hepatitis A ni kimoja wapo kwenye familia ya virusi vya Picornaviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na umbile lenye pande 20 (icosahedral) na ukuta wenye strendi moja ya RNA.
Sifa za kirusi
Kirusi hepatitis A ni aina ya kirusi chenye strendi moja ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Picornaviridae yenye sifa zifuatazo;
Huwa na virusi wadogo wenye ukubwa wa nautikomaili 22 hadi 30nm
Wana umbile lenye pande 20 (ikosahedro)
Wana ukuta wenye strendi moja ya RNA
Ganda lake la njee la seli halijafungwa
Wana kipenyo chanye urefu wa nautikomaili 30
Makundi ya familia ya Picornaviridae
Familia ya Picornaviridae ina genera tano ambazo ni; Enterovirus
Cardiovirus
Aphthovirus
Hepatovirus
Parechovirus
Genera zinazodhuru binadmau ni; Enterovirus
Hepatovirus
Rhinovirus
Utunzwaji wa kirusi
Kirusi hepatitis A hutunzwa na binadamu.
Uenezwaji wa kirusi
Kirusi hepatitis A kinaenezwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia;
Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni
Kutumia maji ya kunywa yenye kirusi
Kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya kirusi hepatitis A
Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya kirusi hepatitis A
Vihatarishi vya maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Hepatitis A ni;
Kusafiri kwenda nchi zenye hali ya juu ya uambukizo ((Afrika, Asia, Mediterranean, Ulaya mashariki, Mashariki ya kati, amerika kusini na kati, Mexico na baadhi ya maeneo ya karibbean)
Mwanaume anayejamiana na mwanaume mwenzake
Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi
Watu walio kwenye mazingira ya kazi yanayowakutanisha na wagonjwa wenye maambukizi ya kirusi hepatitis A
Watu walio kwenye taasisi kubwa
Wagonjwa wenye maambukizi ya kirusi cha UKIMWI
Dalili za maambukizi
Muda wa kuatema ni ndani ya wiki mbili hadi wiki sita. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumwambukiza mtu mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za ugonjwa wa Homa ya ini aina ya Hepatitis A ni;
Homa
Mwili kuchoka
Kupata manjano hasa machoni na kwenye ngozi
Kutapika
Kichefuchefu
Tumbo kuuma hasa upande wa juu wa kulia
Kupoteza hamu ya kula
Viungio vya mwili kuuma
Mwili kuwasha
Kupata mkojo wenye rangi nyeusi
Vipimo tambuzi
Vipimo muhimu kwa aliyeambukizwa kirusi Hepatitis A ni;
Kipimo cha picha nzima ya damu
Kipimo cha Nucleic Acid ya kirusi
Liver function test
Kipimo cha Seroloji
Ultrasonography
Kipimo cha biopsy ya ini
Kipimo cha ugandaji damu
Magonjwa yenye mfanano
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Homa ya ini A kutokana na maambukizi ya kirusi Hepatitis A ni;
Hepatitis E kali
Matibabu ya homa ya ini A
Mgonjwa anatakiwa apate mlo mzuri wenye virutubisho vyote
Mgonjwa atatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana
Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya kuzuia kutapika kama anatapika sana
Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu
Mgonjwa atapandikizwa ini endapo ini lake litakuwa limeharibika.
Kinga
Inaweza kuwa ngumu kujikinga na kirusi huyu, hata hivyo kuna njia mbalimbali unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi;
Nawa mikono baada ya kutoka maliwato na unapogusana na mtu mwenye maambukizi haya (kinyesi, mate n.k)
Kunywa maji safi na salama
Kula vyakula vilivyoiva vema na kutoa mvuke
Kama unahudumia watoto kwenye vituo vya kulelea watoto, hakikisha unanawa mikono mara unapobadilisha nguo mtoto mmoja na kabla ya kwenda kwa mtoto mwingine
Usile vyakula vya mtaani
Safisha matunda kwa maji safi na salama ( unaweza tumia maji yaliyochemshwa)
Kupata chanjo
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
BMC. Hepatitis A Virus. https://bmcinfectdis.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12879-017-2555-x. Imechukuliwa 10/09/2021 2.
MAYO CLINIC. Hepatitis A virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/hepatitis-a/symptoms-causes/syc-20367007. Imechukuliwa 10/09/2021
UPTODATE. Hepatitis A Virus. https://www.uptodate.com/contents/hepatitis-a-virus-infection-treatment-and-prevention#H7718719. Imechukuliwa 10/09/2021
MEDSCAPE. Hepatitis A Virus https://emedicine.medscape.com/article/177484-questions-and-answers. Imechukuliwa 10/09/2021
FDA. Hepatitis A Virus (HAV). https://www.fda.gov/food/foodborne-pathogens/hepatitis-virus-hav. Imechukuliwa 10/09/2021
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:07:27