top of page

Mwandishi;

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri;

Dkt. Benjamin L, MD

7 Aprili 2020 18:16:20

Kirusi Human Papilloma

Kirusi Human Papilloma

Husababisha uvimbe usio saratani wenye jina la papilloma au sunzua kwenye ngozi laini. Kirusi huyu pia huchangia zaidi ya asilimia 80 ya saratani ya shingo ya kizazi licha ya kusababisha saratani zingine pia. Kufanya ngono salama au kupata chanjo hukinga maambukizi ya kirusi huyu.


Familia ya kirusi HPV


Kirusi HPV huwa ni kirusi kimojawapo kwenye familia ya virusi inayoitwa Papovavirus. Vivuri wengine kwenye familia hii ni, polyomaviruses na vacuolating agenti. Kutokana na DNA ya kirusi, kirusi HPV amegawanyika kwenye makundi 16, A hadi P na kwenye haya makundi kuna aina 70 za virusi vya human papilloma.


Mwonekano na umbo


  • Kirusi huwa na sifa zifuatazo

  • Huwa na DNA, bila kuwa na bahasha ya nje

  • Kirusi huwa na kipenyo cha nautikomaili 55 hadi 55

  • Huwa na kapsidi ya icosahedro

  • Jinomu ya kirusi huwa imesokoteka san ana huwa na vipande viwili vya DNA zilizoundana


Uzalishaji wa kirusi


Kirusi huyu huvutiwa na sehemu raini za Ngozi kama midomo na kwenye kifuko cha haja kubwa(mkundu). Kwenye maeneo haya kirusi hujizalia kwa kutengeneza protinina uchafu ambao hufanya Ngozi iinuke na kuonesha uvimbe.


Aina za kirusi Human Papilloma (HPV)


  • HPV 16 na 18 :hawa husababisha aina ya kansa ya mlango wa kizazi

  • HPV 6 na 11 :Hawa husababisha Warts kwenye sehemu za siri

  • Na wengine ni HPV 31, 33, 45, 52 na 55

Magonjwa yanayosababishwa na HPV


Husababisha uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za mwili unaojulikana kama sunzua hasa hasa kwenye maeneo ya siri na mkunduni

Husababisha saratani ya ukuta wa kizazi

Huweza kusabababisha wartsi kwenye sehemu ya haja kubwa


Kirusi HPV hutunzwa na nani ?


Kirusi huyu huweza kutunzwa na binadamu pekee kwenye sehemu laini za mwili kama sehemu za siri na haja kubwa


Uenezwaji wa kirusi


Kirusi cha HPV huenezwa kwa njia ya kufanya ngono mfano


  • Ngono ya uke kwa uke

  • Uke kwa uume

  • Uume kwa uke

  • Uke kwa mdomo

  • Ume kwa njia ya haja kubwa

  • Mdomo kwa njia ya haja kubwa


Unaweza kupata maambukizi hata kama una mpenzi mmoja tu ambaye ana maambukizi ya virusi huyu.


Maambukizi kwa kichanga


Kichanga anaweza kupata maambukizi wakati anazaliwa kwa njia ya uke


Dalili za kuambukizwa


Dalili mara baada ya maambukizi zinaweza zisionekane mpaka miaka kadhaa kupita. Hii inafanya ngumu kutambua ulipata lini maambukizi.


Uamshwaji wa kirusi kilicholala


Kinachoweza kuamsha maambukizi ya kirusi HPV kilicholala kwa muda mrefu ni kushuka kwa kinga ya mwili mfano kwa wagonjwa wa UKIMWI au matumizi ya dawa za kushusha kinga za mwili n.k


Sifa za uvimbe ambao husababishwa na HPV


  • Hauna maumivu

  • Huwa na damu

  • Ni mdogo ambao umejikusanya kwa kundi


Kuna chanjo?


Ndio kuna chanjo ytabaadhiya virusi vya HPV zinazopatikana


Aina ya chanjo inayotolewa

  • 9-valent HPV vaccine (Gardasil® 9, 9vHPV)

  • Quadrivalent HPV vaccine (Gardasil®, 4vHPV)

  • Cervarix


Namna zinavyotolewa


Chanjo ya HPV hutolewa mara mbili (ya kwanza mwezi 0 na inayofuata ni baada ya miezi 6-12) kwa watu walioanza kutumia wakiwa na umri wa miaka 9 hadi 14 na hutolewa kama dozi tatu (yaani chanjo ya kwanza mwezi ziro, ya pili ni baada ya mwezi 1- 2 na ya tatu ni mwezi baada ya kufikisha miezi 6 toka chanjo ya kwanza) kwa walioanza kutumia wakiwa na umri wa miaka 15 hadi 45 na wenye kinga ya mwili dhaifu.


Gardasil 9 hukinga maambukizi ya virusi gani?


Gardasil 9 hukinga virusi vya HPV aina zifuatazo;


  • HPV 6 na 11, wanaosababisha sunzua sehemu za siri kwa asilimia 90

  • HPV 16 na 18 wanaochangia saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 70

  • HPV 31, 33, 45, 52 na 58 wanaochangia saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 10


Cervarix hukinga maambukizi ya virusi gani?


Cervarix hukinga maambukizi ya HPV 16 na 18

Gardasil hukinga maambukizi ya virusi gani?


Gardasil hukinga maambukizi ya virusi HPV 6, 11, 16 na 18


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii



Rejea zamada hii;

  1. Subhash Chandra Parija. Microbiology and immunology. Human papilloma virus.page kurasa ya 469-471 

  2. HealthLineHumanPapillomaVirus. https://www.healthline.com/health/human-papillomavirus-infection. Imechukuliwa 7/4/2020

  3. MedicalNewTodayHPV. https://www.medicalnewstoday.com/articles/246670. Imechukuliwa 7/4/2020

  4. MayoClinicHPV. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/hpv-infection/symptoms-causes/syc-20351596. Imechukuliwa 7/4/2020 5.

  5. MedscapeHPV. https://emedicine.medscape.com/article/219110-overview. Imechukuliwa 7/4/2020

  6. NCI.Human Papillomavirus (HPV) Vaccines. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/risk/infectious-agents/hpv-vaccine-fact-sheet. Imechukuliwa 27.09.2021

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 18:49:39

bottom of page