top of page

Mwandishi;

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri;

Dkt. Mangwella S, MD

16 Septemba 2021 05:58:58

Kirusi Influenza A

Kirusi Influenza A

Kirusi Influenza A ni kirusi anayesababisha homa ya mafua, moja kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hutokea sana kwenye ukanda wa baridi.


Ugonjwa wa kirusi


Kirusi influenza A husababisha ugonjwa wa homa ya mafua kwa biandamu


Ugonjwa wa Homa ya mafua umeanza mwaka gani?


Tafiti zinaonesha janga la homa ya mafua ni moja kati ya janga kubwa kutokea duniani kote. Janga hili lilianza mwaka 1918 na kufikia 1919 likawa limeenea duniani kote. Kwa Tanzania kesi ya kwanza kulipotiwa ilikuwa mwaka 2006.


Kirusi Influenza A kipo katika Familia gani?


Kirusi Influenza A ni kimoja wapo kwenye familia ya Orthomyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha homa ya mafua.


Virusi wengine katika familia ya Orthomyxoviridae


Familia ya Orthomyxoviridae huwa na genera 7 za virusi (baadhi ya rejea zimeainisha genera 5 zinazodhuru binadamu tu) ambazo ni;


  • Alphainfluenzavirus

  • Betainfluenzavirus

  • Influenzavirus C

  • Thogotovirus

  • Isavirus

  • Deltainfluenzavirus

  • Gammainfluenzavirus

  • Quaranjavirus


Kati yao, virusi wanaodhuru binadamu ni pamoja na;


  • Alphainfluenzavirus, kwa jina jingine Kirusi Influenza A

  • Betainfluenzavirus kwa jina jingine Kirusi Influenza B

  • Influenzavirus C

  • Thogotovirus

  • Isavirus


Sifa za kirusi


Influenza A ni moja ya kirusi cha strendi moja ya RNA hasi. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Orthomyxoviridae yenye sifa zifuatazo;


  • Wana RNA moja

  • Ana strendi moja ya RNA hasi

  • Ganda lake la nje ya seli limejifunga

  • Jeni yake ina sehemu nane iliyozungukwa na koti kumi.



Kirusi hutunzwa na nani?


Kirusi Influenza B hutunzwa na binadamu.


Kirusi Influenza A kinaenezwa kwa njia gani?


Kirusi Influenza B kinaenezwa kwa njia zifuatazo;


  • Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua

  • Wakati mwingine watu huambukizwa mafua wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni

  • Kukaa karibu na mtu mwenye maambukizi


Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Influenza A


  • Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya Influenza B

  • Watoto chini ya miaka mitano

  • Watu wanaosafiri ukanda wa baridi

  • Wenye upungufu wa kinga mwilini

  • Watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama vile asthma, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, kisukali na magonjwa ya ini


Dalili za ugonjwa wa Homa ya mafua


Muda wa kuatema ni ndani ya siku moja hadi nne. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za ugonjwa wa Homa ya mafua ni;


  • Kuchuruzika kwa kamasi

  • Homa

  • Kikohozi kikavu

  • Kukosa hamu ya kula

  • Macho kuwa mekundu na kutoa majimaji

  • Maumivu ya mwili

  • Mwili kuchoka na kulegea

  • Maumivu ya misuli

  • Uchovu

  • Kushindwa kupumua vizuri

  • Kuhisi baridi na joto

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi


Vipimo


Vipimo vya kirusi Influenza A;


  • RT-PCR

  • Kuotesha kirusi

  • Hesabu ya chembe zote nyeupe za damu

  • Kiwango cha madini mwilini

  • Quick voe influenza A+B test

  • Stat flu

  • Radiografia ya kifua


Magonjwa yanayofanana


Magonjwa yanayoweza kufanana dalili za maambukizi yakirusiinfluenza A ni pamoja na;


  • Homa ya Dengue

  • Ugonjwa wa Corona (UVIKO)

  • Maambukizi ya Cytomegalovirus

  • Adeno virus infection

  • Sindromu ya Upumuaji wa shida (ARDS)

  • Maambukizi ya Arenaviruses

  • Kirusi influenza C na B


Matibabu


  • Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa

  • Mgonjwa atapatiwa maji ya kutosha kwa njia ya mishipa au kunywa

  • Mgonjwa anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika

  • Mgonjwa atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa

  • Mgonjwa anayepata shida ya upumuaji na kuonekana oxygen yake imeshuka atapata oxygen

  • Mgonjwa atapata dawa kwaajiri ya maambukizi ya virusi ambazo ni Baloxavir, Marboxil, Oseltamivir, Peramivir na Zenamivir


Kinga na chanjo


Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;


  • Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu

  • Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye

  • Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka

  • Pata chanjo ya Influenza A kwa wakati sahihi

  • Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote


Je kuna chanjo ya kirusi Influenza A?


Chanjo kwa ajiri ya virusi vya Influenza A ipo na hutolewa kwa mtu anayekuwa kwenye vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi cha Influenza A.


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

​

Orodha kuu


Rejea zamada hii;

  1. CDC. Influenza A virus. https://www.cdc.gov/flu/about/viruses/index.htm. Imechukuliwa 14/09/2021. 

  2. WHO. Influenza A virus. https://www.who.int/health-topics/influenza-seasonal#tab=tab_1. Imechukuliwa 14/09/2021. 

  3. MAYO CLINIC. Influenza A virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/flu/diagnosis-treatment/drc-20351725. Imechukuliwa 14/09/2021. 

  4. MEDSCAPE. Influenza A virus. https://emedicine.medscape.com/article/219557-overview. Imechukuliwa 14/09/2021. 

  5. Science direct. Influenzavirus C. https://www.sciencedirect.com/topics/veterinary-science-and-veterinary-medicine/influenzavirus-c. Imechukuliwa 14/09/2021. 

  6. Science direct. Orthomyxoviridae. https://www.sciencedirect.com/topics/immunology-and-microbiology/orthomyxoviridae. Imechukuliwa 14/09/2021.

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:13:19

bottom of page