Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L, MD
16 Septemba 2021 05:13:32
Kirusi Influenza B
Kirusi Influenza B ni moja ya kirusi anayesababisha homa ya mafua na maambukizi yake hutokea sana kwenye ukanda wa baridi na hudhuru sana watoto.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi influenza B husababisha homa ya mafua isiyokali.
Ugonjwa wa Homa ya mafua umeanza mwaka gani?
Tafiti zinaonesha janga la homa ya mafua inayosababishwa na kirusi influenza B ni moja kati ya janga kubwa kutokea duniani kote. Janga hili lilianza mwaka 1918 na kuenea duniani kote kufikia mwaka 1919 wakati Tanzania Kwa Tanzania kesi ya kwanza kulipotiwa ilikuwa mwaka 2006.
Kirusi cha Influenza B kipo katika Familia gani?
Kirusi Influenza B ni kimoja wapo kwenye familia ya Orthomyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha homa ya mafua.
Sifa za kirusi
Kirusi Influenza B ni virusi vya RNA hasi.Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Orthomyxoviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana RNA moja
Ana strendi moja ya RNA hasi
Ganda lake la njee la seli limejifunga
Jeni yake ina sehemu nane iliyozungukwa na koti kumi
Virusi wengine katika familia ya Orthomyxoviridae
Familia ya Orthomyxoviridae huwa na genera 7 za virusi (baadhi ya rejea zimeainisha genera 5 zinazodhuru binadamu tu) ambazo ni;
Alphainfluenzavirus
Betainfluenzavirus
Influenzavirus C
Thogotovirus
Isavirus
Deltainfluenzavirus
Gammainfluenzavirus
Quaranjavirus
Kati yao, virusi wanaodhuru binadamu ni pamoja na;
Alphainfluenzavirus, kwa jina jingine Kirusi Influenza A
Betainfluenzavirus kwa jina jingine Kirusi Influenza B
Influenzavirus C
Thogotovirus
Isavirus
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Influenza B hutunzwa na binadamu.
Kirusi Influenza B kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Influenza B kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua
Wakati mwingine watu huambukizwa mafua wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni
Kukaa karibu na mtu mwenye maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Influenza B
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya Influenza B
Watoto chini ya miaka mitano
Watu wanaosafiri ukanda wa baridi
Wenye upungufu wa kinga mwilini
Watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama vile asthma, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, kisukali na magonjwa ya ini
Dalili za ugonjwa wa Homa ya mafua
Muda wa kuatema (incubation period) ni ndani ya siku moja hadi nne. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za ugonjwa wa Homa ya mafua ni;
Pua kutoa uchafu (makamasi)
Kupata homa
Kikohozi kikavu
Kukosa hamu ya kula
Macho kuwa mekundu na kutoa majimaji
Kichwa kuuma
Mwili kuchoka na kulegea
Maumivu ya misuli
Mwili kuchoka
Kushindwa kupumua vizuri
Kuhisi baridi na joto
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Vipimo
Vipimo vya kirusi Influenza B;
RT-PCR
Kuotesha kirusi
Hesabu ya chembe zote nyeupe za damu
Kiwango cha madini mwilini
Quick voe influenza A+B test
Stat flu
Radiografia ya kifua
Magonjwa yanayofanana
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Homa ya mafua ni pamoja na;
Homa ya Dengue
Ugonjwa wa Corona (UVIKO)
Maambukizi ya Cytomegalovirus
Adeno virus infection
Sindromu ya Upumuaji wa shida (ARDS)
Maambukizi ya Arenaviruses
Matibabu
Matibabumaranyingi hulenga kupunguzamakalitadali kwa;
Kupatiwa maji ya kutosha kwa njia ya mishipa au kunywa
Kupumzika
Panadol kwa ajiri ya maumivu na homa
Mgonjwa anayepata shida ya upumuaji na kuonekana oxygen yake imeshuka atapata oxygen
Mgonjwa atapata dawa kwaajiri ya maambukizi ya virusi ambazo ni Baloxavir, Marboxil, Oseltamivir, Peramivir na Zenamivir
Kinga na chanjo
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka
Pata chanjo ya Influenza A kwa wakati sahihi
Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote
Je kuna chanjo ya kirusi Influenza B?
Chanjo kwa ajiri ya virusi vya Influenza B ipo na hutolewa kwa mtu anayekuwa kwenye vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi cha Influenza B.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
CDC. Influenza B virus. https://www.cdc.gov/flu/about/viruses/types.htm. Imechukuliwa 14/09/2021.Â
WHO. Influenza B virus. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/influenza-(seasonal). Imechukuliwa 14/09/2021.Â
NCBI. Influenza B virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK22148/. Imechukuliwa 14/09/2021.Â
Science direct. Influenzavirus C. https://www.sciencedirect.com/topics/veterinary-science-and-veterinary-medicine/influenzavirus-c. Imechukuliwa 14/09/2021.Â
Science direct. Orthomyxoviridae. https://www.sciencedirect.com/topics/immunology-and-microbiology/orthomyxoviridae. Imechukuliwa 14/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:14:02