Mwandishi;
Dkt Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L ,MD
17 Septemba 2021 08:16:03
Kirusi Influenza C
Kirusi Influenza C ni kirusi kinachosababisha homa ya mafua isiyokali inayotokea sana kwa watoto. Homa ya mafua ni moja kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hutokea sana kwenye ukanda wa baridi.
Ugonjwa wa kirusi
Kirusi influenza C husababisha homa ya mafua isiyokali hasa kwa watoto.
Historia ya homa ya mafua
Tafiti zinaonesha janga la homa ya mafua ni moja kati ya janga kubwa duniani kote. Janga hili lilianza mwaka 1918 na kufikia 1919 janga hili likawa limeenea duniani kote. Kwa Tanzania mgonjwa wa kwanza kulipotiwa ilikuwa mwaka 2006.
Familia ya kirusi Influenza C
Kirusi Influenza C ni kimoja wapo kwenye genus ya influenza virus C na familia ya Orthomyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha homa ya mafua.
Sifa za kirusi
Kirusi Influenza C ni moja ya kirusi chenye strendi moja ya RNA hasi kwenye familia ya virusi vya Orthomyxoviridae ambacyo huwa na sifa zifuatazo;
Wana RNA moja
Ana Strendi moja ya RNA hasi
Ganda lake la njee la seli limejifunga
Jeni yake ina sehemu saba iliyozungukwa na koti tisa.
Virusi wengine katika familia ya Orthomyxoviridae
Familia ya orthomyxoviridae huwa na genera 7 (baadhi ya waandishi wameandika genera tano tu zinazodhuru binadamu) za virusi ambazo ni;
Alpha influenza virus
Beta influenza virus
Delta influenza virus
Gamma influenza virus
Isavirus
Thogotovirus
Quaranjavirus
Influenza C virus
Kati yao virus wanaodhuru binadamu ni pamoja na;
Alpha influenza virus, kwa jina jingine ni Influenza A
Beta influenza virus, kwa jina jingine ni Influenza B
Influenza virus C
Thogotovirus
Isavirus
Utunzwaji
Kirusi Influenza C hutunzwa na binadamu.
Uenezaji wa kirusi
Uenezwaji wa kirusi Influenza C awali ni kupitia mfumo wa hewa, kwa namna ifuatavyo;
Kirusi anaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kwa kupatwa na matone ya maji kutokwa kwa mgonjwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua
Wakati mwingine watu huambukizwa kirusi huyu kwa kugusa maeneo ambayo mwathirika ameyagusa na haswa endapo ukitia mikono kinywani au kwenye pua
Kukaa karibu na mtu mwenye maambukizi kiasi cha kupumiliana
Vihatarishi vya maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Influenza C ni;
Mtu yeyote ambaye hajapata chanjo ya Influenza
Watoto chini ya miaka mitano
Watu wanaosafiri kwenda ukanda wa baridi
Wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini
Watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama vile pumu, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, kisukali na magonjwa ya ini
Dalili za kuambukizwa
Muda wa kirusi kuatema ni kuanzia siku moja hadi nne. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana na hujumuisha;
Kutokwa kamasi
Kupata homa
Kikohozi kikavu
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya kula
Kuhisi baridi na joto
Vipimo
Vipimo vya kirusi Influenza C
RT-PCR
Kuotesha kirusi
Picha nzima ya damu
Kiwango cha madini mwilini
Zstat flu
Radiografia ya kifua
Magonjwa linganifu
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Homa ya mafua ni pamoja na;
Oma ya Dengue
Ugonjwa wa Corona
Maambukizi ya Cytomegalovirus
Maambukizi ya kirusi Adeno
Sindromu ya upumuaji wa shida(ARDS)
Maambukizi ya Arenaviruses
Matibabu
Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa.
Mgonjwa atapatiwa maji ya kutosha kwa njia ya mishipa au kunywa
Mgonjwa anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mgonjwa atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa
Mgonjwa anayepata shida ya upumuaji na kuonekana oxygen yake imeshuka atapata oxygen
Mgonjwa atapata dawa kwa ajiri ya kudhibiti uzalianaji wa kirusi kama Baloxavir, Marboxil, Oseltamivir, Peramivir na Zenamivir
Kinga na chanjo
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi
Ukiugua, usitoke nyumbani isipokuwa kama unaenda kutafuta husuma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa tishu au kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka
Pata chanjo ya Influenza A kwa wakati sahihi
Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote
Je kuna chanjo ya kirusi Influenza C?
Tafiti zinaonesha hakuna chanjo ya kirusi influenza C lakini inashauriwa mtu kupata chanjo ya kirusi influenza A na B ambazo zitasaidia kujikinga na maambukizi.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
NCBI. Influenza C virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7019359/. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Sciencedirect.com. Influenza C virus. https://www.sciencedirect.com/topics/biochemistry-genetics-and-molecular-biology/influenza-c-virus. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
W. Paul Glezen, MD. Influenza C Virus Infection. https://jamanetwork.com/journals/jamainternalmedicine/article-abstract/600319. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Gaitonde. Influenza: Diagnosis and Treatment. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/31845781/. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Rodney S. Daniels, et al. Molecular Characterization of Influenza C Viruses from Outbreaks in Hong Kong SAR, China. https://journals.asm.org/doi/10.1128/JVI.01051-20. Imechukuliwa 15/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:11:16