Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. benjamin L, MD
23 Septemba 2021, 10:15:44
Kirusi mumps
Kirusi mumps ni kirusi kinachosababisha ugonjwa wa mumps kwa jina jingine matumbwitumbwi.
Ugonjwa wa kirusi mumps umeanza mwaka gani?
Tafiti zinaonesha ugonjwa wa mumps (matumbwitumbwi) unaosababishwa na kirusi mumps ulianza kuonekana kwa mara ya kwanza mwaka 1945.
Kirusi mumps kipo katika Familia gani?
Kirusi mumps kipo katika genus ya Rubivirus na familia ya Paramyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha homa na matumbwitumbwi.
Sifa za kirusi
Mumps ni kirusi cha strendi moja ya RNA hasi. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya paramyxoviridae. Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana RNA moja
Strendi RNA hasi
Ukuta wa njee ya seli umefunga
Wana kipenyo cha 150-300nm
Virusi wengine kwenye familia ya kirusi cha Mumps
Virusi wengine katika familia ya paramyxoviridae ni;
Kirusi para influenza
Kirusi measles (surua)
Kirusi respiratory syncytial
Mtunzaji wa kirusi
Kirusi mumps hutunzwa na binadamu.
Ueneaji wa kirusi
Kirusi mumps kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua
Wakati mwingine watu huambukizwa mumps wanapogusa mate ya mtu mwenye maambukizi
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi mumps;
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo
Wasafiri wa kimataifa
Watu ambao kinga ya mwili imeshuka
Dalili za maambukizo ya kirusi mumps
Muda wa kuatema ni ndani ya siku 16 hadi 18. Mtu mwenye maambukizi ya kirusi mumps huweza kumwambukiza mtu mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana; Dalili za ugonjwa za kuambukizwa kirusi mumps ni pamoja na;
Homa
Mwili kudhoofika
Maumivu karibu na sikio kuelekea mashavuni
Maumivu ya kichwa
Uso kuvimba
Kupoteza uwezo wa kusikia
Vipimo
Vipimo vya kutambua na kuwezesha matibabu ya maambukizi ya kirusi mumps ni;
Asilimia kubwa ya vipimo ni kwa kumuangalia mgonjwa
Immunoglobulin G (1g G)
Immunoglobulin M (1g M)
Serum amylase
Kuotesha kirusi
Picha nzima ya damu
CT-Scan
Magonjwa yanayofanana na maambukizi ya kirusi mumps
Encephalitis
Measles
Myocarditis
Maambukizi ya HIV kwa mtoto
Homa ya uti wa mgongo kwa mtoto
Homa ya ubongo kwa mtoto (encephalitis)
Rubella kwa mtoto
Pertussis
Matibabu
Hakuna tiba ya kuponya kirusi mumps, matibabu yanayotolewa ni kudhibiti dalili tu na yanaweza kuhusisha;
Kupatiwa dawa za maumivu na homa
Kupatiwa dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kama yameambatana na kirusi
Kunywa maji ya kutosha
Kupata muda mwingi wa kupumzika
Pia mtoto atatakiwa apate chanjo
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Pata chanjo ya mumps kwa wakati sahihi
Nawa mikono mara kwa mara
Je kuna chanjo ya kirusi mumps?
Chanjo kwa ajiri ya kirusi mumps ipo na mtoto anatakiwa apate chanjo kwa wakati sahihi.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
CDC. Mumps virus. https://www.cdc.gov/vaccines/pubs/pinkbook/mumpshtml#epidemiolog. Imechukuliwa 22/09/2021.
Mayoclinic. Mumps virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/mumps/diagnosis-treatment/drc-20375366. Imechukuliwa 22/09/2021.
NCBI. Mumps virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK8461/. Imechukuliwa 22/09/2021.
Medscape. Mumps virus. https://reference.medscape.com/article/966678-overview. Imechukuliwa 22/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:08:00