Mwandishi;
ULY CLINIC
Mhariri;
27 Machi 2020, 10:55:19

Kirusi Polio
Kirusi polio ni kirusi kilicho kweye familia ya Picornaviridae , familia hii huwa na sifa za kuwa na virusi wadogo, wasio na ukuta nje, na wenye RNA moja yenye sensi . Kuna Genera 13 za familia hii mpaka sasa zinafahamika ambazo ni Aphtovirus, Erbovirus, Teschovirus, Sapelovirus, Senecavirus, Tremovirus, Avihepatovirus, Cardiovirus, Hepatovirus, Cosavirus, Parechovirus, Kobuvirus na Enterovirus. Genera sita za mwisho hujulikana kusababisha magonjwa kwa binadamu.
Genera ya kirusi enterovirus
Kirusi polio kipo kwenye genera ya enterovirus.
Aia za virusi vya polio
Kuna aina tatu za kirusi polio aina 1, 2 na 3
Sifa za kirusi polio
Ni kirusi cha kwanza kuweza kutakaswa na kupatikana kwenye mfumo vipande vidogo vya kristo
Huwa na umbo la mpira na kipenyo cha nautiko maili 27
Huwa na viunda 60, kila kiunda kina protini 4
Genomu ya kirusi huwa na RNA moja yenye sensi chanya ya RNA
Magonjwa yanayosabaishwa na polio
Magonjwa yanayosabaishwa na polio ni;
Meninjaitizi ya aseptiki
Kupooza
Homa iziyotofautishwa
Unenezaji wa kirusi
Kirusi huyu huenezwa kwa kula chakula au maji yaliyochanganyika na kinyesi au kunywa maji yaliyo na kirusi.
Pathofiziolojia ya ugonjwawa polio
Kirusi anapoingia mwili huanza kujizalia kwenye ukuta wa nyuma kati ya koo na pua (nasofalinksi) na myukosa ya gastrointestino. Kirusi huwa na upinzani kwenye tindikali, nyongo na vimeng’enya mbalimbali vya mfumo wa Gastrointestino na hivyo huwa hakidhuriwi. Kirusi polio kinapoingina mwilini huanza kujizalisha mara dufu kwenye tezi ya tonsili na kiunga cha payers kilicho kwenye iliamu.
Baada ya kujizalia husambaa kwenye damu na wengine huingia kwenye tishu za retikuloendothelia na kujizalisha kwa wingi kisha kuingia kwenye kwenye damu. Kirusi polio hupenda kujishikiza kwenye mishipa ya fahamu ya uti wa mgongo hivyo kupelekea uharibifuwa mishipa hiyo sehemu kirusi alipojishikiza na dalili ya kupooza huonekana.
Kupooza kutokana na maambukizi ya kirusi polio hakusabaishwi na kirusi kudhuru misuli bali kudhurika kwa mishipa ya fahamu. Kirusi huyu pia hudhuru shina la ubongo na kusababisha kupooza kwa misuli ya upumuaji.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii;
Subhash Chandra Pariji. Microbiology and Immunology Textbook toleo la 2 kurasa 498, 513-514 imechukuliwa 27.03.2020
Sabine M.G. van der Sanden Prevalence and Genetic Diversity of Human Enteroviruses in the Context of Poliovirus Eradication pg 10. Imechukuliwa 27.03.2020
Paul JR (1971). A History of Poliomyelitis. (Yale studies in the history of science and medicine). New Haven, Conn: Yale University Press. ISBN 978-0-300-01324-5.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:19:03