Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Sospeter B, MD
19 Septemba 2021, 13:54:49
Kirusi Rota A
Kirusi Rota A ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa ya kuharisha inayoambatana na kuharisha sana hasa kwa watoto. Kirusi huyu hudhuru ukuta wa epithelia uliofunika kwa ndani ya utumbo mwembamba.
Kirusi Rota A kimeanza mwaka gani?
Tafiti zinaonesha kuwa Askofu na wenzake ndio walikuwa wa kwanza kugundua kirus rota A kwa mara ya kwanza mwaka 1972 walipoona kwa hadubini kirusi chenye umbile la ringi kwenye haja kubwa ya mtoto mwenye homa kali ya matumbo huko Australia.
Genus na familia ya kirusi Rota A
Kirusi Rota A ni kimoja wapo kwenye genus ya Rota virus na familia ya Reoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi mbili ya RNA pia husababisha Homa ya matumbo kwa watoto.
Sifa za kirusi
Rota A ni moja ya kirusi cha strendi mbili ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Reoviridae. Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana RNA mbili
Ana Strendi mbili ya RNA
Ukuta wa juu ya seli yake umefungwa na shelled capsid mbili
Wana umbile la duara (wheel)
Wana kipenyo cha 70nm
Genome yake ina segment 11
Genera za Kirusi rota A
Reoviridae imegawanyika katika genera nane;
Orthoreovirus
Coltivirus
Rotavirus
Orbivirus
Aquareoviru
Cypovirus
Phytoreovirus
FijivirusÂ
Genera zinazopatikana kwa binadamu ni;
Orthoreovirus
Coltivirus
Rotavirus
Orbivirus
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Rota A hutunzwa na binadamu.
Kirusi Rota A kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Rota A kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni
Kutumia maji ya kunywa au chakula chenye vimelea
Kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono baada ya kutoka chooni
Watoto kugusa sehemu chafu pia kupeleka mdomoni bila kunawa mikono
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Rota A
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya kirusi Rota A hasa watoto.
Watoto wenye miezi 3 hadi 35
Watu ambao umri umeenda sana
Watu wazima wanaolea watoto wenye maambukizi
Dalili
Dalili za homa ya kuharisha kutoka na maambukizi ya kirusi Rota A huanza kuonekana ndani ya siku mbili baada ya mtu kupata maambukizi. Dalili hizo ni;
Kuharisha choo chenye majimaji na wakati mwingine damu kidogo.
Kupata homa
Tumbo kuuma
Kukosa hamu ya kula
Mwili kukosa nguvu na kuchoka
Ishara mbaya za kuharisha zinazotakiwa kukufanya kuonana na daktari haraka;
Mdomo kukauka
Miungurumo ya tumbo kuongezeka
Macho kuingia ndani
Ngozi inapovuta kwa kufinya kujirudi taratibu sana
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kupungua uzito
Vipimo vya kirusi Rota A
Kuotesha kirusi
Picha nzima ya damu
Kiwango cha madini kwenye damu
Kipimo cha haja kubwa
Latex agglutination
Enzyme immune Assay
Magonjwa yanayofanana na Rota A
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na homa ya matumbo ni pamoja na;
Giardiasis
Kuishiwa maji kwa mtoto
Gastroenteraitiz
Gastroenteraitiz ya watoto
Maambukizi ya salmonella kwa watoto
Matibabu ya Ugonjwa wa homa ya kuharisha
Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya ugonjwa wa homa ya kuharisha, ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;
Hakikisha njia ya hewa, upumuaji na mzunguko wa damu uko vizuri
Mtoto atapatiwa ORS kwaajiri ya kunywa au kuongezewa maji kwenye mishipipa kama ana upungufu mkali wa maji. Maji huwa na madini sodium, potassium, chloride na kalisiamu kwa njia ya mshipa
Mtoto anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mtoto atapata panadol kushusha homa
Mtoto atapatiwa madini Zinc ili kupunguza kuharisha na kuponya utumbo
Mtoto atapatiwa dawa za kuzuia kutapika kama anatapika sana
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;
Pata chanjo ya kirusi Rota A kwa wakati sahihi
Nawa mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote hasa mara baada ya kuingia na kutoka chooni
Nawa mikono ya watoto mara kwa mara kwa maji safi na sabuni
Zingatia usafi kwa ujumla
Je kuna chanjo ya kirusi Rota A?
Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rota A ipo. Kuna chanjo aina mbili ambazo ni Rotateq inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 32 na Rotarix inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 24.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
Mayo clinic. Rota A virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/rotavirus/diagnosis-treatment/drc-20351306. Imechukuliwa 17/09/2021.Â
NCBI. Rota A virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK8558/. Imechukuliwa 17/09/2021.Â
CDC. Rota A virus. https://www.cdc.gov/rotavirus/index.html. Imechukuliwa 17/09/2021.Â
Medscape. Rota A virus. https://emedicine.medscape.com/article/803885-overview. Imechukuliwa 17/09/2021.Â
Sciencedirect. Rota A Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/rotavirus. Imechukuliwa 17/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:10:08