Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Mangwella S, MD
19 Septemba 2021, 14:27:28

Kirusi Rota B
Kirusi Rota B ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa kali ya kuharisha na kutapika kwa watoto na watu wazima.
Kirusi Rota B kimeanza mwaka gani?
Tafiti zinaonesha kuwa kirusi Rota B kilionekana kwa mara ya kwanza mwaka 1982 uko China, kisha kikaonekana uko India mwaka 1998 na mwaka 2000 kikaonekana Bangladesh.
Kirusi Rota B kipo katika Familia gani?
Kirusi Rota B ni kimoja wapo kwenye genus ya kirusi Rota na familia ya Reoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi mbili ya RNA pia husababisha homa ya kuharisha na kutapika kwa watoto na watu wazima.
Sifa za kirusi
Rota B ni moja ya kirusi cha strendi mbili ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Reoviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana RNA mbili
Ana Strendi mbili ya RNA
Ukuta wa juu ya seli yake umefungwa na shelled capsid mbili
Wana umbile la ringi
Wana kipenyo chenye urefi wa 70nm
Genome yake ina vpande 11
Familia Reoviridae
Familia Reoviridae ina spishi tisa moja wapo akiwa kirusi rota A ambazo ni;
Kirusi rota A
Kirusi rota B
Kirusi rota C
Kirusi rota D
Kirusi rota E
Kirusi rota F
Kirusi rota G
Kirusi rota H
Kirusi rota I
Spishi Zinazosababisha ugonjwa kwa binadamu ni;
Kirusi Rota A
Kirusi Rota B
Kirusi rota C
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Rota A hutunzwa na binadamu.
Kirusi Rota B kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Rota B kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni
Kutumia maji ya kunywa au chakula chenye vimelea
Kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono baada ya kutoka chooni
Watoto kugusa sehemu chafu pia kupeleka mdomoni bila kunawa mikono
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Rota B
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya kirusi Rota
Watoto wadogo
Watu ambao umri umeenda sana
Watu wazima wanaolea watoto wenye maambukizi
Dalili za ugonjwa wa homa ya kuhara
Dalili za homa ya kuhara huonekana ndani ya siku mbili baada ya mtu kupata maambukizi ambazo ni;
Kuharisha choo chenye majimaji na wakati mwingine damu kidogo.
Kupata homa
Kutapika
Tumbo kuuma
Kukosa hamu ya kula
Mwili kukosa nguvu na kuchoka
Ishara mbaya zinazoweza kuonekana kwa mgonjwa;
Mdomo kukauka
Miungurumo ya tumbo kuongezeka
Macho kuingia ndani
Ngozi inapovutwa kurejea taratibu kwenye hali yake ya kawaida
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kupungua uzito
Vipimo vya kirusi Rota B
Picha nzima ya damu
Kiwango cha madini kwenye damu
Kipimo cha haja kubwa
Latex agglutination
Enzyme immune Assay
RT-PCR
Magonjwa yanayofana na Dalili za Rota B
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na homa ya matumbo ni pamoja na;
Giardiasis
Kuishiwa maji kwa mtoto
Gastroenteraitiz inayohitaji matibu ya dharura
Maambukizi ya salmonella kwa motto
Matibabu
Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya ugonjwa kuhara na kutapika kutokana na maambukizi ya kirusi rota B, ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;
Hakikisha njia ya hewa, upumuaji na mzunguko wa damu uko vizuri.
Mtoto atapatiwa ORS kwaajiri ya kunywa kama ana dalili kiasi au za wastani za kuishiwa maji au
Kuongezewa maji yenye madini sodium, potassium, chloride na calcium kwa njia ya mshipa kama ana upungufu mkali wa maji wilini
Mtoto anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mtoto atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa
Mtoto atapatiwa Zinc ya watoto ili kuharakisha uponyaji wa tumbo na kupunguza kuharisha
Mtoto atapatiwa dawa za kuzuia kutapika kama anatapika sana
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;
Pata chanjo ya kirusi Rota A kwa wakati sahihi
Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote hasa mara baada ya kuingia na kutoka chooni
Nawa mikono ya watoto mara kwa mara kwa maji safi na sabuni
Zingatia usafi kwa ujumla
Chanjo
Je kuna chanjo ya kirusi Rota B? Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rota B ipo. Kuna chanjo aina mbili ambazo ni Rotateq inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 32 na Rotarix inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 24.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
Rejea zamada hii;
Takeshi Sanekata sanekata, et al. Human group B Rotavirus Infections Cause Severe Diarrhea in Children and Adult. https://journals.asm.org/doi/10.1128/JCM.41.5.2187-2190.2003. Imechukuliwa 17/09/2021.
MSD. Rota B virus. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/immunization/rotavirus-vaccine#v39242815. Imechukuliwa 17/09/2021.
Medscape. Rota B virus. https://emedicine.medscape.com/article/803885-overview. Imechukuliwa 17/09/2021.
Science direct. Rota B Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/rotavirus-b. Imechukuliwa 17/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:09:34