Sehemu hii utajifunza kuhusu Virusi ambao wanaleta magonjwa mbalimbali kwa binadamu
Kirusi Human Papilloma
Licha ya kusababisha uvimbe usio usio saratani kama sunzua kwenye ngozi, huchangia zaidi ya asilimia 80 ya saratani ya shingo ya kizazi licha ya kusababisha saratani zingine pia. Jikinge na maambukizi ya kirusi huyu kwa kupima, kufanya ngono salama na kupata chanjo.
Kirusi Influenza A ni kirusi anayesababisha homa ya mafua, moja kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hutokea sana kwenye ukanda wa baridi.
Kirusi Influenza C ni kirusi kinachosababisha homa ya mafua isiyokali inayotokea sana kwa watoto. Homa ya mafua ni moja kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hutokea sana kwenye ukanda wa baridi.
Kirusi measles au kirusi cha surua ni moja ya kirusi kwenye familia ya Paramyxoviridae kinachosababisha ugonjwa wa surua. Surua ni moja kati ya magonjwa ya kuambukizwa, asilimia 90 ya maambukizi hutokea kama mtu ana magonjwa mengine au kinga yake ya mwili imeshuka.