Kirusi Rino au rhinovirus, ni kirusi chenye RNA kutoka kwenye familia ya Picornaviridae. Kirusi huyu huongoza kusababisha homa ya baridi kwa binadamu kwa kuathiri sana pua na koo.
Kirusi Rota ni aina ya kirusi chenye RNA katika familia ya Reoviridae. Kirusi huyu huongoza kusababisha ugonjwa wa kuharisha kwa watoto wachanga na watoto wadogo karibia duniani kote.
Kirusi Rota A ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa ya kuharisha inayoambatana na kuharisha sana hasa kwa watoto.