Kirusi Rota C ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa ya kutapika na kuharisha (gastroentaraitiz) isiyo kali haswa kwa watoto wenye umri mkubwa.
Kirusi Rubella ni aina ya kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Rubella. Kirusi hiki husababisha homa na vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani.
Kirusi Varicella Zosta (VZV) ni kirusi ambacho husababisha magonjwa ya tetekuwanga na mkanda jeshi, kirusi huyu yupo kwenye Familia ya virusi inayoitwa Herpesi Viridae
Kirusi cha UKIMWI ni kirusi ambacho kitiba kinaitwa Humman Immunodeficiency Virus au HIV kama watu wengi wanavyo fahamu na kwa lugha ya kiswahili huitwa Virusi Vya UKIMWI, kifupisho chake VVU.