Sehemu hii utajifunza kuhusu Virusi ambao wanaleta magonjwa mbalimbali kwa binadamu
Kirusi chikungunya
Kirusi chikungunya ni kirusi anayesababisha homa ya homa ya chikungunya, moja kati ya magonjwa ya mlipuko yanayotokea sana kwenye ukanda wa sana kwenye ukanda wa tropiki kama Afrika na kusini mashariki mwa Asia pamoja na India.
Kirusi herpes simplex (HSV), ni kirusi kilicho kwenye familia ya Herpesviruses, Familia hii ina virusi wengine ambao ni kirusi varicellazoster, Kirusi cytomegaly, kirusi Epstein–Barr na kirusi human herpes 8- kisababishi cha sakoma ya Kaposi’s.
Kirusi human parainfluenza ni kirusi kinachosababisha maambukizi katika mfumo wa upumuaji hasa kwa watoto. Maambukizi hayo ni kama mafua yenye homa, laryngotracheobronchitis , bronkolaitiz na nimonia.
Kirusi zika ni kirusi anayeenezwa kwa mbu aina ya aedes, mara nyingi huwa hasababishi ugonjwa mkali na dalili zake kuu ni homa, maumivu ya kichwa, misuli, maungio ya mwili na macho mekundu.
Kuna aina mbili za virusi vya UKIMWI, VVU-1 na VVU-2, VVU-1 ambavyo hupatikana karibia duniani kote huwa na kasi ya kusababisha UKIMWI zaidi ya VVU-2 ambavyo hupatikana Afrika Magharibi.