Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic
Vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa maziwa kwa mama baada ya kujifungua
​
Uzalishaji wa maziwa hutegemea vitu vingi ikiwa pamoja na namba ya idadi unavyonyonyesha ama kukamua maziwa kwa ajili ya mtoto, na kiasi cha chakula unachokula. Ingawa wamama wengi huzalisha kiwango cha maziwa ya kutosha, hakuna kipimo kina weza kuoonyesha maziwa yako yanatoka kwa wingi kiasi gani cha kumtosha mtoto.
​
Kuna baadhi ya vyakula vya asili kama pilipili manga n.k vinaweza kuongeza uzalishaji wa maziwa endapo zikitumiwa kwa wingi. Pilipili manga ni mojawapo ya kiungo kinachoongeza uzalishaji wa maziwa.
Vyakula vingine
Baadhi ya vyakula huongeza uzalishaji wa maziwa, hivyo vyakula hivi huwa na faida wakati wa kipindicha kunyonyesha .
Karoti, viazi vitamu, vitunguu swaumu, tangawizi, pilipili manga, mboga za majani-kama spinachi, kabeji,sukuma wiki
Radha ya maziwa yanayozalishwa huwa haibadiliki sana, hata hivyo hutegemea aina ya chakula ulichokula kwawakati mwingine, mfano umekula chakula chenye pilipili manga, maziwa yanaweza kuwana na radha kama unayopata kutokana na kula pilipili manga
Bonyeza hapa kuendelea kusoma kuhusu 'Ni wakati gani baada ya kujifungua mama huanza kutoa maziwa?'
​
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri wa daktari kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ya afya yako.
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020