Vyakula vya kuepuka ili usipate tumbo
​
1 Pombe
​
Baadhi ya vinywaji vyenye pombe huwa vina nishati nyingi, nishati hii huwa kwa kiasi kikubwa kiasi kuliko mahitaji ya mwili. Hata hivyo pombe huongeza hamu ya kula na pia huzuia ubongo kupata taarifa kutoka kwenye tumbo kwamba umeshiba, na hivyo kunywa pombe kunakusababisha kula zaidi. Unaweza kukumbuka kwamba kila unapokunywa pombe lazima ule kitu kingine kama nyama n.k
Pombe pia hupunguza mwili kutumia nishati mwilini, nishati hii hubidi kuhifadhiwa kwenye mwili kama mafuta chini ya tumbo n.k Kunywa pombe zaidi kutakufanya kunenepa zaidi.
​
Endapo unaenda kwenye sherehe au maeneo ya kufurahisha na ukataka kupata kilevi kidogo, chagua kinywaji aina ya wine au bia bila kula vitu vingine, ingawa uwe makini maana pombe ni hatari ikitumiwa kwa kiwango zaidi ya kilichoshauriwa.
Fikilia mara mbili kabla hujanywa pombe
​
Soda
​
Kila mtu anawezekana ameshawahi kunywa soda katika maisha yake, soda zipo za aina nyingi ikiwa zile zimeandikwa kuwa hazina sukari ambazo zimekuwa zikitumika kwa watu wenye kisukari. Soda huwa na sukari nyingi, soda moja imekadiliwa kuwa na sukari ya vijiko 12 vya chai, kunywa soda moja ni sawa na mtu aliyekula vijiko 12 vya sukari. Sukari hii hutoa nishati ya kilo kalori 150mwilini. Endapo umekula chakula na kuongeza soda utakuwa umepitiliza mahitaji ya mwili na hivyo nishati hii inayobaki mwili huibadilisha kuwa mafuta na kuihifadhi chini ya tumbo.
​
Hata hivyo soda huongeza gesi tumboni, kuzuia mwili usitumie sukari, hii inaweza kusababisha unene na kujaa kwa tumbo.
​
Endapo utabadili mawazo ya kutotumia soda na kuchagua kunywa juisi za kununua kwenye supermarket, utakuwa hujamaliza tatizo la kuongezeka tumbo kwani juisi nyingi katika supermarket huwa hazina virutubisho na vitamin kwa afya ya mwili bali huwa na sukari kwa wingi pamoja na ladha ya tunda ambayo unayofikilia. Cha kufanya andaa juisi ya matunda hlisi au kunywa maji ya kutosha kwa afya ya mwili wako
Pelemende na bablish/Bazoka
​
Ukitafuna bablishi huongeza hali ya mtu kupata njaa hasa ya vyakula vyenye sukari, hii ndio maana baada ya kula pipi au bigijii iliyoandikwa kuwa ina kemikali ya mint, ukila chakua, kunywa maji au kitu ambacho hakina sukari utahisi ladha mbaya.
​
Vyakula vyenye Chumvu nyingi
​
Chumvi huwa muhimu sana kwenye mwili, husaidia katika uendeshaji wa kazi mbalimbali ndani ya mwili. Chumvi huwa na tabia ya kuhifadhi maji mwilini ambapo hukufanya uvimbe mwili endapo utatumia kwa wingi. Watu wengi kwa siku hutumia chumvi zaidi ya miligramu 3400 mara mbili zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwa afya (1500). Epuka chumvi ya kuongezea baada ya kupika chakula, usiache kabisa kutumia chumvi kwani ni hatari, mwili unatakiwa kupata chumvi ili kuwa na afya njema. Endapo unataka ushauri kuhusu chumvi unaweza kuongea na daktari wako au kuwasiliana nasi kupitia namba za huduma kwa wateja.
​
Vyakula vya kupikwa kwa haraka na vya kukaanga
​
Vyakula vinavyoitwa “fast food” huwa na nishati kwa wingi inayokuweka hatarini kupata tatizo la uzito kupita kiasi. Nishati hii huhifadhiwa kama mafuta kwenye tumbo na kukusababishia tumbo kujaa na kuwa na mwonekano mbaya.
Vyakula vya kukaanga huwa na mafuta mengi, vyakula hivi hufanya kazi kama sponji kwa kufyonza mafuta na kisha huingi akwenye mfumo wa damu. Mafuta haya husababisha tumbo kujaa na kitambi. Vyakula hivi vyenye mafuta mengi pia huzawadia ubongo(bonyeza kusoma) na kusababisha unenepe sana kwa kuwa utavitaka mara kwa mara.
​
Mayoneizi(mayonnaise)
Watu wengi hutumia mayonaizi kuweka kwenye chakula kama chipsi na kachumbali ili kuongeza radha. Asilimia 80 ya Mayoneizi huwa mafuta, na kijiko kimocha cha mayoneizi huwa na nguvu za kalori 100. Ukitumia vijiko vingi zaidi maanake unahifadhi nguvu nyinig zaidi katika mwili ambazo hazitumiki na kisha kusababisha unenepe.
​
Ice cream
Ice cream huwa na mafuta na sukari kwa wingi, mafuta ya ice cream huhifadhiwa kwenye tumbo. Mafuta yanayohifadhiwa husababisha tumbo kuwa kubwa, hata hivyo ulaji wa ice creame huleta mazoea ya kutaka mara kwa mara kama wanavyokuwa watu wanaoachishwa madawa ya kulevya. Endapo unapenda ice cream basi unaweza tengeneza yako mwenyewe kwa kusaga ndizi mbivu moja ndogo kisha kuigandisha, na kuila, hapa utapata nguvu kiasi isiyozidi kalori 100 ukifananisha na ice cream.
​
Vyakula vinavyofanya tumbo lijae gesi
Vyakula vinavyofanya tumbo lijae gesi au kuhisi chakula hakijameng'enywa na hali ya kuwa umeshiba huwa si vizuri. Vyakula hivi vingi ni vile ambavyo vina mchanganyiko wa maziwa pamoja na maziwa yenyewe. Tufaa au apple huwa na tabia hiyo pia, ni vema ukaepuka vyakula vinavyokufanya hivi ili kukwepa kuwa na tumbo kubwa. Unaweza fanya mazoezi yatakayosaidia kumenge'enywa kwa chakula endapo umekula vyakula vyenye tabia hii.
​
Vyakula ambavyo vimeandikwa kwamba havina sukari
​
Vyakula au vinywaji ambavyo havina sukari hutumika kwa watu wenye kisukari, ingawa vyakula hivi huwa havina sukari aina ya glucosi, huwa na sukari aina ya polyalcohol ambayo husaidia kwa namna moja watu wenye kisukari tu. Endapo hauna kisukari ni vema ukaepuka vyakula na vinywaji hivi kwa sababu vyakula hivi hukusababishia upate hamu ya kuvila mara kwa mara na kukuletea kuongezeka uzito kupita kiasi.
​
Chagua kula vyakula halisia kuwa mbadala wa vyakula vya kununua vilivyo na madhara kwenye afya yako
Sehemu hii Imezungumzia kuhusu;
​
Mabadiliko ya mwili unapopunguza uzito
Mambo ya kujua kabla ya mazoezi
Namna ya kuendelea kufanya mazoezi bila kuacha au kama huna mda
Namna ya kutumia chakula kupunguza uzito bila mazoezi
Maandalizi ya kufanya kabla ya mazoezi
Vyakula vya kuepuka usipate tumbo kubwa