Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
​
(Yuticaria)-Urticaria
Yutikaria ni neno lililotokana na neno la kilatini cha kisasa urticaria. Neno Urticaria limetokana na mmea mmoja unaoitwa urtica wenye sindano ndogo sana inayoweza kuchoma ngozi na kusababisha uvimbe wa kama mtu aliyeng'atwa na mdudu au nyuki.
Maana
​
Ugonjwa huu wa ngozi hudumu kwa muda mfupi, mara nyingi chini ya masaa 24. Tatizo hili huweza kusababishwa na maambukizi, au mzio kwenye chakula na dawa na mara nyingi sababu huwa haijulikani sana kwa wagonjwa.
Yutikaria husababisha kuvimba na kuwasha na kuwa nyekundu kama vile umeng’atwa na mdudu.
Ugonjwa huu unaweza kuambatana na matatizo mengine kama Vaskulaitis, pamfigoid, na dermataitis ya hepatifomis
Endapo umeona una dalili hizi wasiliana na daktari wako. Unaweza kupata ushauri na tiba kutoka kwa madaktari wa ULY CLINIC kwa kubonyeza hapa au Hapa
​
Soma zaidi kuhusu, Aina Yutikaria, Visababishi, Matibabu
​
Nenda kwenye magonjwa mengine ya ngozi kwa kubonyeza hapa